1).Elikyesia - Kuzaliwa.
Historia ya Bibi Elikyesia.Bibi Elikyesia Nsero Salema Kileo alizaliwa mwaka 1890 akiwa mtoto wa kwanza wa Nsero Salema Kileo.Nsero alikuwa na wake wawili, Elikyesia alikuwa mtoto wa kwanza wa mke mkubwa. Nsero alikataa kubatizwa kwa madai kwamba haoni tofauti kati ya aliyebatizwa na asiyebatizwa.Mtoto wa mdogo wake Nsero anaitwa Nkanturu naye alikataa kubatizwa.2).Ndoa .
3).Kubatizwa.
5).Vita ya Dunia.
Mwaka 1916 alikwenda vitani (vita kuu ya kwanza 1916-19). Wakati wanarudi toka vitani walitembea toka Posta-Dsm hadi Moshi Nyumbani, walianza safari watu 7 lakini walifika wawili naye akiwa mmoja wao, na alipofika akaoa bibi Elikyesia 1920.Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) .
Mzee Elinewinga Menda Nnyaka alimaliza safari yake mwaka 1984 akiwa na uzee mwema wa miaka 114 na rekodi bora kabisa (Nndumi Narumishwa Nde na Ma!) .
4. Elinewinga Maana yake nini.
Elinewinga maana yake ni Bwana alinifanya kuwa mshindi! Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) Wanaoniheshimu nitawaheshimu na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu! (1 Sam.2:30 ).
.Kwa hili kila mtu ajitafakari ni kivipi anamheshimu Bwana,utafiti wa haraka waonyesha wote waliomheshimu Bwana waliacha watu baada yao sio "Maraami"(angalia kila lilipofika kanisa na pale ambapo halikufika watu wake wakoje?).Kama unawapenda watoto wako jifunze kumheshimu Bwana naye atasimama na wanao Mwa. 26:2-5, Zab.112:2 (wazao wake watakuwa hodari) .
Kweli tunaona huyu babu amekuwa Eli newinga kwelikweli (Bwana amemfanya mshindi) amelitendea haki hili jina na wazao wake wamekuwa hodari duniani.
6).Bibi Elikyesia Katokea wapi?.
6a) Watoto wa Salema -Elianshitaua,Nsero,Ndesamburo7).Bibi Elikyesia na ndugu zake.
7). Elinewinga na Uongozi.
Mwaka 1936 mzee Elinewinga Nnyaka alichaguliwa kuwa 'Nshili' (Kiongozi) wa Lukani na Ng'uni na baadae aliongezewa eneeo la Kyuu. Akiwa 'Nshili' alishawishi wananchi wa Lukani,Ng'uni na Kyuu kushika mashamba na kulima katika maeneo ya Yuri,Sufi na Lawate ambayo yalikuwa mapori. Yeye mwenyewe alionyesha mfano kwa kushika mashamba ya kutosha ambayo mpaka leo wajukuu wengi wamemilikishwa ! Akiwa Nshili wa Maeneo haya alifungua barabara za mitaa yote ya maeneo hayo! Vile vile alichaguliwa kuwa Bwana shamba wa eneo lote la Masama.