1.Menda Meturumu Nnyaka.

Menda ni mtoto wa Nnyaka Meturumu.Menda aliishi pale Urereny,pale kwa Ndesamburo pale anakoishi Boronga kwa Bibi Makitika, mke wake Meenda(Shammesariyo) ni dada yake na Nderanguso. Nderanguso ni Baba yake na Shilesario, Major,Shilekirwa Munuo . Ndugu zake na Meenda (watoto wa Nnyaka) ni Gabriel, Kuninike na Meshili .Watoto wa Menda Nnnyaka ni Elineshikwa, Mangatari, Ndesamburo, Shitirinsiande na Mankwe .

2.Ndugu zake Meenda na watoto wao

2a).Watoto wa Kuninike ni Jubilate,Manyara,Fredrick , Michael.

2b).Watoto wa Meshili ni Elifasi na Kafii.

3. Meturumu - Historia.

Meturumu (Babu yake na Meenda ) alitokea Kenya pamoja na ndugu zake wakifikia maeneo ya Mesarani(Pata Historia ya wachagga na Natai kwenye link juu). Wengine walikwenda Siha wakaitwa Kihundwa.Yeye Meturumu aliendelea mbele akafikia maeneo ya Lukani kupita Kinarini. Eneo hilo la Meturumu ndiko kwenye chanzo cha maji tunayotumia Lukani hadi KIA. .

Meturumu alipofika eneo la Meturumu alitengeneza mfereji mkubwa(Nfongo wa Meturumu) toka chanzo cha mto Namwi, yeye akajenga bondeni na mfereji ukapita juu ili aweze kuutumia.Baada ya muda alisafiri kwenda kuona ndugu zake akiacha familia, akiwa safarini Kipindi cha masika mfereji ulifurika na kuharibu kila kitu ikiwepo familia ambayo iliangamia kwa maji

Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) .

Mzee Elinewinga Menda Nnyaka alimaliza safari yake mwaka 1984 akiwa na uzee mwema wa miaka 114 na rekodi bora kabisa (Nndumi Narumishwa Nde na Ma!) .

4. Elinewinga Maana yake nini.

Elinewinga maana yake ni Bwana alinifanya kuwa mshindi! Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) Wanaoniheshimu nitawaheshimu na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu! (1 Sam.2:30 ).

.

Kwa hili kila mtu ajitafakari ni kivipi anamheshimu Bwana,utafiti wa haraka waonyesha wote waliomheshimu Bwana waliacha watu baada yao sio "Maraami"(angalia kila lilipofika kanisa na pale ambapo halikufika watu wake wakoje?).Kama unawapenda watoto wako jifunze kumheshimu Bwana naye atasimama na wanao Mwa. 26:2-5, Zab.112:2 (wazao wake watakuwa hodari duniani) .

4a).Je Elinewinga alimheshimu Bwana?.

Yee Mmbee!Mwaka 1922 Alishirikiana na Hayati Mwl. Zakaria Swai (Babake na Veraeli Swai) pamoja na watu wengine wa Lukani kuanzisha nyumba ya sala Lukani. Baadae hii nyumba ya sala ilikuja kuzaa usharika wa Lukani ambapo alikuja kuchaguliwa kuwa mzee wa kanisa.

Kweli tunaona huyu babu amekuwa Eli newinga kwelikweli (Bwana amemfanya mshindi) amelitendea haki hili jina na wazao wake wamekuwa hodari duniani.

.

4b).Elinewinga amaliza Vizuri

Mzee Elinewinga Menda Nnyaka alimaliza safari yake mwaka 1984 akiwa na uzee mwema wa miaka 114 na rekodi bora kabisa (Nndumi Narumishwa Nde na Ma!) .

5.Meturumu aacha Laana!

. Meturumu alipokuta familia ime angamia kwa mafuriko alipanda mti wa mfumu katikati ya ule mto akisema kamwe hautakaa tena uwepo mfereji pale (Kuanzia wakati huo hata sasa kumekuwa na juhudi kadhaa za kufufua mfereji huo lakini zimefeli.Kulikuwa na Project kubwa kabisa miaka ya karibuni ikitengewa mamilioni ya pesa (watu wa Lukani wanafahamu kilichoendelea)

6.Elinewinga aliongoza kwa Haki.

Barnaba Ngalami Mmari alikuwa akiishi pale Rawashi jirani na Mchungaji Barnaba Munuo. Huyu Barnaba Ngalami ni Babu yake na Mchungaji Barnaba.Barnaba Ngalami alikuwa mfugaji mahiri sana kipindi hicho na mifugo ilinona sana. Kama kawaida ya ufalme (uMangi) kitu chochote kizuri ni cha mfalme(Mangi). Huwezi kula mbuzi yako nzuri iliyonona hiyo ni ya Mangi!. Mangi alikuwa na 'Njama' wapambe. Hawa kazi yao ni kupita na kuangalia nani ana kitu kizuri na kukichukua kwa Mangi. Hawa walipokuja kwa Barnaba na kuona mifgo minono, walipeleka taarifa na Mangi akatuma watu kuchukua, yeye alikataa na kusema Mangi kama anataka mbuzi au ng'ombe nono afuge wa kwake. Mangi alipopelekewa hizi taarifa alikasirika sana na kutoa amri Barnaba angamizwe na kila alichonacho. Mzee Elinewinga akiwa Nchili ndiye aliyetakiwa kuongoza zoezi hilo. Lakini kabla ya zoezi kutendeka alimtuma kijana, mzee Aleendwa Natai(miaka hiyo alikuwa kijana) ampelekee taarifa hizo usiku na usiku huo huo Barnaba Mmari aliondoka na familia yake na mifugo kuelekea Siha na baadae waliekea huko Meru maeneo ya Sangisi. Elinewinga na jeshi lake walipokwenda pale kesho yake walikuta Boma tupu.Baada ya miaka kadhaa kupita Mtoto wa kwanza wa Elinewinga alikuja kuoa mjukuu wa kwanza wa Barnaba Ngalami, wakati huo Barnaba alishafariki

7).Je Ndugu zake Elinewinga ni nani? .