1.Kuzaliwa -Mzee Elinewinga

Elinewinga Menda Nnyaka alizaliwa wakati wa Ifumu lya Saiye hii ni kabla ya 1871.Alizaliwa Nkwantana kijiji cha Ng'uni. Walihama kutoka Ng'uni kwenda Lukani mpakani -Forest, baadae walihama hapo na kwenda kuishi Kisawe (Kisawe ni pale kwa Amani wa Zebedayo). Walihama tena hapo Kisawe na kwenda Urereny na baadae kabisa walihamia Nkumbi ambapo ndipo alipoishi maisha yake yote hakuhama tena .

1b).Kuwa Mkristo.

Mzee Elinewinga alibatizwa mwaka 1925 usharika wa Masama akiwa na miaka 75

2.Mzee Elinewinga apigana vita kuu ya Dunia.

Mwaka 1916 alikwenda vitani (vita kuu ya kwanza ya Dunia 1916-19). Wakati wanarudi toka vitani walitembea toka Posta-Dsm hadi Moshi Nyumbani, walianza safari watu 7 lakini walifika wawili naye akiwa mmoja wao.

2a).Ndoa.

Mzee Elinewinga M. Meturumu alifunga ndoa na Elikyesia Nsero mwaka 1920 akiwa na miaka 50 .

Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) .

Mzee Elinewinga Menda Nnyaka alimaliza safari yake mwaka 1984 akiwa na uzee mwema wa miaka 114 na rekodi bora kabisa (Nndumi Narumishwa Nde na Ma!) .

3. Elinewinga Maana yake nini.

Elinewinga maana yake ni Bwana alinifanya kuwa mshindi! Na kweli tumeona Bwana alimfanya kuwa mshindi kwelikweli,Haleluya! (Zab.60:12) Wanaoniheshimu nitawaheshimu na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu! (1 Sam.2:30 ).

.

Kwa hili kila mtu ajitafakari ni kivipi anamheshimu Bwana,utafiti wa haraka waonyesha wote waliomheshimu Bwana waliacha watu baada yao sio "Maraami"(angalia kila lilipofika kanisa na pale ambapo halikufika watu wake wakoje?).Kama unawapenda watoto wako jifunze kumheshimu Bwana naye atasimama na wanao Mwa. 26:2-5, Zab.112:2 (wazao wake watakuwa hodari) .

4.Je Elinewinga alimheshimu Bwana?.

Yee Mmbee!Mwaka 1922 Alishirikiana na Hayati Mwl. Zakaria Swai (Babake na Veraeli Swai) pamoja na watu wengine wa Lukani kuanzisha nyumba ya sala Lukani. Baadae hii nyumba ya sala ilikuja kuzaa usharika wa Lukani ambapo alikuja kuchaguliwa kuwa mzee wa kanisa.

5. Elinewinga achaguliwa kuwa Kiongozi wa Serikali(Nshili).

Mwaka 1936 mzee Elinewinga Nnyaka alichaguliwa kuwa 'Nshili' (Kiongozi) wa Lukani na Ng'uni na baadae aliongezewa eneeo la Kyuu. Akiwa 'Nshili' alishawishi wananchi wa Lukani,Ng'uni na Kyuu kushika mashamba na kulima katika maeneo ya Yuri,Sufi na Lawate ambayo yalikuwa mapori. Yeye mwenyewe alionyesha mfano kwa kushika mashamba ya kutosha ambayo mpaka leo wajukuu wengi wamemilikishwa ! Akiwa Nshili wa Maeneo haya alifungua barabara za mitaa yote ya maeneo hayo! Vile vile alichaguliwa kuwa Bwana shamba wa eneo lote la Masama.

6. Elinewinga alipataje 'Ushili'.

Elinewinga hakuwa kwenye familia ya utawala kwa yeye kupewa 'ushili' . Huu uongozi aliupata baada ya 'Nshili' aliyekuwepo kupoteza kodi(Hawa viongozi ndio waliokuwa wanasimamia kodi ktk maeneo yao, na hapa tuna ona Ndelimo akipoteza nafasi yake ya uongozi na kuchukuliwa na Elinewinga. Ndelimo alikuwa kabla ya Elinewinga.

7.Tarehe 25/03/1960 - Mzee Elinewinga alipanda mti pale Kinariny akasema mti huu tumeupanda uunganishe ukoo wote .

8.Mwaka huo huo wa 1960, Wazee wafuatao walikutana Losaa 1).Veranndumi,2).Alenaufoo 3).Jacob(Yaakobo) walikaa usiku kucha wakifanya recording, walifanya mahojiano na kutengeneza mkanda wa Historia ya ukoo na wachagga kwa ujumla (Kanda hii tuliisikiliza kule Kinariny kwenye kikao cha ukoo).

WATOTO WA MEENDA.